Ee mama yetu Maria,
Twaomba sana ee mama
Usituache gizani
kwa mwanao tuombee (2 volte)
- Mama yetu Maria, utusikilize
Sisi wana wako, tunaosumbuka
Maisha yetu mama, hayana furaha
Tujaze neema, tupate faraja
Ee mama yetu Maria,
Twaomba sana ee mama
Usituache gizani
kwa mwanao tuombee (2 volte)
- Utuombee kwake, mwanao mpendwa
Atutie nguvu, tushinde maovu
Dunia ina giza, dunia ni ngumu
Bila nguvu yake, hatuwezi kitu
Ee mama yetu Maria,
Twaomba sana ee mama
Usituache gizani
kwa mwanao tuombee (2 volte)
- Tuombee Maria, tuombee mama
Ili wana wako, tufike mbinguni
Ee mama yetu Maria,
Twaomba sana ee mama
Usituache gizani
kwa mwanao tuombee (2 volte)